Cha kutumaini sina
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Cha kutamaini sina, ila damu yake Bwana,
sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha;
Kwake Yesu nasimama,
ndiye mwamba ni salama,
Ndiye mwamba ni salama.
Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga nguvu zake ndiyo nanga.
Damu yake na sadaka, nategemea daima,
yote chini yakiisha mwokozi atanitosha.
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani;
nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook