Njooni Wachungaji Bethlehemu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Njooni wachungaji
Bethlehemu!
Njooni kumtazama
mtoto mzuri.
Mwana wa Mungu
amezaliwa.
Baba amtuma atukomboe.
Msiogope!
Twende Bethlehemu
tukaone
tulivyoambiwa na malaika.
Tuyaonayo tutatangaza
na kutukuza kwa
nyimbo nzuri
Haleluya!
Kweli malaika
wametangaza
Furaha kubwa kwa
wachungaji.
Sasa po pote
patengenezwa.
Furahini!


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook