Sifuni Nyote Huruma
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Sifuni nyote huruma ya
Mungu,
kwa nyimbo nzuri,
umati wa Yesu!
Atualika furahani:
/: Msifuni Bwana kwa
neema yake!:/
Yeye ni Mfalme
anayetawala;
viumbe vyote
vinamtumikia,
hata malaika
wamuabudu,
/: wanamwimbia kwa
sauti nzuri.:/
Enyi mataifa, hofu
iacheni!
Njooni kwa Yesu,
Mchunga kondoo
mwema.
Sikilizeni Neno lake:
/: Atukomboa kwa kufa
kwake.:/
Awapa watu chakula chochote, atushibisha kama baba mzuri, aleta jua hata mvua, /: atubariki kwa wema wake.:/
Sifuni wote huruma ya
Mungu,
kwa nyimbo nzuri,
umati wa Yesu!
Sasa huzuni twaishinda:
/: Msifuni Bwana kwa
neema yake:/


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook