Yesu kwetu ni rafiki
What a friend we have in Jesus!
Tenzi za rohoni ( #9 ) , Nyimbo standard ( #239 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;
tukiomba kwa Babaye, maombi asikiya;
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;
kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia.
Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia.
Haifai kufa moyo, dua atasikia.
Hakuna mwingine mwema, wa kutuhurumia;
atujua tu dhaifu; maombi asikia.
Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,
ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.
Watu wangekudharau, wapendao dunia,
hukwambata mikononi, dua atasikia.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook