Siku ya Mbingu kujawa na Sifa.
Tenzi za rohoni ( #94 ) , Nyimbo standard ( #249 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Siku ya Mbinguni kujawa na sifa, dhambi zilizidi duniani; Yesu akaja azaliwe mtu, awe na watu ulimwenguni.
Alinipenda, alinifia, ameondoa na dhambi zangu; alifufuka nipewe haki, yuaja tena Mwokozi wangu.
Na siku moja walikwenda naye, wakamkaza msalabani; Aliumia, aliaibishwa, ili atuokoe dhambini.
Siku hiyo wakamlaza chini, kaburini alipumzika; matumaini yetu wenye dhambi, ni mwokozi, kwake twaokoka.
Kaburini likashindwa kumshika; jiwe likatoka mlangoni, alifufuka kwa kushinda kwake, naye yuko milele mbinguni.
Siku moja atatujia tena; utukufu wake tutaona; atawaleta na wapenzi wetu; mwokozi; wangu, tutaonana.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook