Taji Mvikeni
Tenzi za rohoni ( #8 ) , Nyimbo standard ( #185 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Taji mvikeni, taji nyingi tena, kondoo mwake kitini, Bwana wa maBwana; Nami tamsifu, alikufa kwangu, ni mfalme mtukufu, mkuu wa Mbingu.
Taji mvikeni, Mwana wa bikira; Anazovaa kichwani, aliteka nyara; Shiloh wa wanabii, mchunga wa watu, shina na tanzu vya Yese, wa Bethilehemu.
Taji mvikeni, Bwana wa mapenzi; Jeraha zake ni shani, ni vito vya enzi, Mbinguni hakuna hata malaika awezaye kuziona, pasipo kushangaa.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook