Wamwendea Yesu kwa kusafiwa
Are you washed in the blood of the lamb
Tenzi za rohoni ( #80 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
je neema yake atumwagia,
tumeoshwa kwa damu ya kondoo?
Kuoshwa, kwa damu,
itutakasayo ya kondoo;
ziwe safi nguo nyeupe mno;
umeoshwa kwa damu ya kondoo?
Wamwandama daima mkombozi,
na kuoshwa na damu ya kondoo?
yako kwa msulubiwa makazi,
umeoshwa kwa damu ya kondoo?
Atakapokuja Bwana -arusi,
Uwe safi kwa damu ya kondoo!
Yafae kwenda mbinguni mavazi,
Yafuliwe kwa damu ya kondoo.
Yatupwe yaliyo na takataka,
na uoshwe kwa damu ya kondoo.
Huoni kijito chatiririka,
na uoshwe kwa damu ya kondoo?

Wamwendea Yesu kwa kusafiwa -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook