Wakristo Iwekeni Mioyo Tayari
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Wakristo, iwekeni
mioyo tayari.
Yesu awaingie,
ni mwokozi wenu.
Mungu amemtuma
kwa neema na rehema,
atuletee sisi
uzima na nuru
Mwokozi anakuja,
mlimieni njia!
Mioyo iwe safi
acheni matendo
yanayomchukiza.
Lijazwe kila bonde,
milima ipunguzwe
mioyoni mwenu.
Ukiwa mnyenyekevu,
wapendwa na Mungu.
Ukiwa na kiburi,
utaangamizwa.
Ukimtumikia,
Mungu kwa Mwendo
mwema
umpendezao yeye,
Yesu akupenda.
Uniweke tayari niliye maskini, Ee Yesu siku hizi kwa rehema yako. Ingia moyoni, ukinijia sasa. Nami nitakusifu kwa kinywa na moyo


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook