Twasoma ni Njema Sana
Tenzi za rohoni ( #104 ) , Nyimbo standard ( #207 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, vinanda vizuri viko, na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana.
Siku zote ni mchana, ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, ni nchi ya raha; walioko wanuona, uso wa Mwokozi, tena jua jingine hapana, ni nchi ya raha.
Nyama na vitu viovu havimo kabisa; kifo nacho, na ubovu, havimo kabisa. Ni watakatifu wote, wameoshwa dhambi zote; wasiosafiwa wote hawamo kabisa.
Tuna dhambi, pia sote, mwokozi akafa; kwake tutaoshwa zote, mwokozi akafa; kwake twapata wokovu, tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa.
Baba, mama, ndugu zetu, twendeni kwa Bwana; huku chini sio kwetu, twendeni kwa Bwana; tusishikwe na dunia, na dhambi kutulemea; tutupe vya chini pia, twendeni kwa Bwana.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook