Yote Namtolea Yesu
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Yote namtolea Yesu,
nampa moyo wote,
nitampenda siku zote,
namwandama kila saa.
Yote kwa Yesu,
yoye kwa Yesu,
yote kwako, Ee mwokozi,
natoa sasa.
Yote namtolea Yesu,
nainamia pake;
nimeachana na anasa,
kwako Yesu nipokee.
Yote namtolea Yesu,
nifanye niwe wako;
nipe roho yako, Bwana,
anilinde daima.
Yote namtolea Yesu,
nami naona sasa,
furaha ya ukombozi;
nasifu jina lake.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook