Mahali ni pazuri
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Mahali ni pazuri, ndugu wanapokaa,
wakipatana vema, na wakipendana.
Kama umande mzuri, unyweshavyo shamba,
vivyo na Mungu wetu, hubariki ndugu.
Upendano hujenga, boma zuri kwao,
wakae na amani, waliookakoka.
Na ulimwengu wote, watiwa nuruni,
halafu kundi moja, na mchunga mmoja tu.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook